// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NIYONZIMA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA KWANZA CHA LWANDAMINA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NIYONZIMA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA KWANZA CHA LWANDAMINA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 10, 2016

    NIYONZIMA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA KWANZA CHA LWANDAMINA YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima hayumo kabisa katika kikosi cha Yanga kinachomenyana na JKU ya Zanzibar jioni ya leo katika mchezo wa kirafiki.
    Kocha Mzambia, George Lwandamina amepanga kikosi chake cha kwanza Yanga leo kwa ajili ya mchezo na timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi na Niyonzima hayumo kabisa kwa sababu ni mgonjwa.
    Haruna Niyonzima (kushoto) hayumo kabisa katika kikosi cha Yanga kinachomenyana na JKU ya Zanzibar jioni ya leo katika mchezo wa kirafiki

    Lwandamina aliyechukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi, amewapanga; Ally Mustafa 'Barthez', Hassan Kessy, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Said Juma, Juma Mahadhi, Matheo Antony, Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Geoffrey Mwashuiya.
    Katika benchi Lwandamina aliyeanza kazi Yanga wiki mbili zilizopita amewaweka Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent 'Dante', Simon Msuva, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Justin Zulu, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Deus Kaseke na Kelvin Yondani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYONZIMA HAYUMO KABISA KIKOSI CHA KWANZA CHA LWANDAMINA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top