Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU za kanda ya Ziwa, Mbao FC na Mtibwa Sugar zinamenyana na kesho Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza katika mchezo maalumu wa kirafiki kutoa heshima kwa marehemu Ismail Khalfan.
Khalfan, mchezaji wa timu ya vijana Mbao alifariki dunia Desemba 4, mwaka huu wakati akiiitumikia timu yake ya vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Marehemu Ismail Khalfan alifariki dunia Desemba 4, mwaka huu akiichezea timu ya vijana ya Mbao FC
Mbali ya kutoa heshima kwa marehemu Khalfan, pia waratibu wa mchezo huo wakiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), wamepanga mapato yake yote ni kutoa rambirambi kwa familia ya Khalfan iliyopoteza ndugu yao mchezoni.
TFF, KRFA, MZFA na wadau wengine wangali wakitoa pole kwa familia kwa msiba kwa familia kwa msiba wa Ismail Khalfan ambaye pia ameombolezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Rais wa CAF, Issa Hayatou.
Kadhalika, mchezo huo utatumika kama kuzipima nguvu timu hizo baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) hivyo wadau wote wa michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuchagia rambirambi ya familia hiyo ambayo kwa pamoja na wanafamilia ya soka walipoteza hazina nyingine muhimu kwenye mpira wa miguu.

0 comments:
Post a Comment