// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 21, 2016

    LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA

    KIUNGO mshambuliaji wa Liberty Professionals, Latif Blessing amechaguliwa Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Ghana msimu wa 2015/2016. 
    Winga huyo machachari ambaye alikuwa ana msimu mzuri na klabu hiyo ya Accra, amewapiku viungo Kwasi Donsu wa Medeama na Abdul Bashiru wa Dream FC kushinda tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika Ijumaa iliyopita mjini Accra. 
    Blessing pia alishinda tuzo ya mfungaji bora wa msimu wa Ligi Kuu y Ghana kwa mabao yake 17 aliyofunga. 
    Mchezaji wa Hearts of Oak, Inusah Musah ameshinda tuzo ya beki bora wakati mlinda mlango Richard Ofori wa mabingwa wa Ligi,  Wa All Stars amekuwa kipa bora.
    Mchezaji Bora na mfungaji bora wa Ligi ya Ghana, Latif Blessing wa Liberty Professionals (kushoto) akipokea tuzo yake

    WASHINDI WOTE WA TUZO
    Mchezaji Bora wa Msimu -   Latif Blessing (Liberty Professionals)
    Mfalme wa Mabao - Latif Blessing (Liberty Professionals)
    Kipa Bora wa Msimu - Richard Ofori (Wa All Stars)
    Beki Bora wa Msimu  - Inusah Musah (Hearts of Oak)
    Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu - Abdul Alidu Hudu
    Klabu Bora ya Msimu - Wa All Stars (kwa kushinda taji la ligi)
    Kocha Bora wa Msimu - Anos Adipa (Wa All Stars)
    Mtendaji Mkuu Bora wa Msimu - Oduro Nyarko (Wa All Stars)
    Tuzo ya mchezo wa kiungwana- Berekum Chelsea
    Refa Bora wa Msimu - Awal Mohammed
    Mpiga picha Bora wa Msimu - Paul Agbeyagah
    Kamisaa Bora wa Msimu -  Augustine Asante
    Mshika Kibendera Bor wa Msimu -  Haruna Bawa
    Tuzo ya heshim- Welbeck Abra-Appiah (Mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya Ligi)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LATIF BLESSING NDIYE MFALME WA SOKA NA MABAO GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top