Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO James Agyekum Kotei ‘Lampard’ leo jioni ameanza majaribio katika klabu ya Simba kwenye kambi ya Morogoro.
Kocha Mcameroon, Joseh Marius Omog atakuwa na siku mbili za kumuangalia vizuri James Kotei aliyezaliwa Agosti 10, mwaka 1993 kabla ya kutoa majibu kwa uongozi kwamba asajiliwe au la.
Mchezaji huyo ambaye mara ya mwisho msimu uliopita alichezea Al-Oruba SC ya Ligi Kuu ya Oman, alitua chini jana jioni kutoka kwao, Ghana na leo asubuhi amepelekwa kambini Morogoro.
Kotei aliyezaliwa mjini Accra, Ghana, kisoka aliibukia timu ya watoto ya Corner Babies F.C ya mjini Kumasi mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka tisa tu na mwaka 2007, akahamia akademi ya Golden Foot ambako alicheza hadi mwaka 2009.
James Agyekum Kotei ‘Lampard’ wakati anawasilijana tayari kwa majaribio katika klabu ya Simba
Soka ya ushindani Kotei alianza kucheza mwaka 2010 katika klabu ya Liberty Professionals F.C. ya Dansoman na moja kwa moja akawa kivutio kwa uchezaji wake na kupewa jina “Unbeatable James” au “James Lampard” akifananishwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa England, Frank Lampard aliyewika Chelsea kwa miongo miwili iliyopita.
Msimu wa 2010–2011 ulikuwa mzuri zaidi kwa kiungo huyo kwenye Ligi Kuu ya Ghana baada ya kufanikiwa kujikusanytaia mashabiki wengi kutokana na uchezaji wake mzuri.
Na kwake huo ukawa wakati mwafaka kuanza kutafuta maisha nje ya Ghana, baada ya kutimkia Oman mwaka 2015 akijiunga na Al-Oruba SC, ambako Septemba 8, mwaka jana alicheza mechi yake ya kwanza katika sare ya 1-1 na Muscat Club kwenye mchezo wa Kombe la Ligi Oman, maarufu kama Oman Professional League Cup.
Alicheza mechi yake ya Ligi Kuu Septemba 13 mwaka jana katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Salalah SC na pia akacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Sultan Qaboos Desemba 30, mwaka 2015 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya mahasimu wakubwa, Sur SC.

0 comments:
Post a Comment