Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Al Suwaiq ya Oman, Kipre Herman Tchetche amesema kwamba Simba imefanya kosa kumuacha kipa Vincent Angban na watamkumbuka.
Akizungumza na Nipashe jana kutoka Oman, mshambulaji huyo wa zamani wa Azam FC alisema kwamba Simba imeacha kipa mzuri ambaye angewasaidia kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya muda mrefu.
“Angban ni kipa mzuri sana. Na naamini alikuwa anaelekea kuwapa Simba ubingwa wa kwanza baada ya miaka mingi, lakini nimeshangazwa sana na habari za kumuacha, ila watamkumbuka,”alisema Tchetche.
Hadi mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu unafikia tamati mapema mwezi huu, Angban ndiye aliyekuwa kipa mwenye rekodi nzuri zaidi, akifungwa mabao sita tu katika mechi 15, lakini ajabu ameachwa na kusajiliwa Daniel Agyei kutoka Medama SC ya Ghana.
Vincent Angban ameachwa Simba licha ya kudaka vizuri mzunguko wa kwanza
Angban pia aliweka rekodi ya kudaka mechi sita mfululizo bila kufungwa. Baada ya kufungwa katika sare ya 1-1 na Yanga Oktoba 1, mwaka huu – Angban akadaka mechi tano mfululizo zilizofuata bila kuruhusu bao, Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine, 2-0 na Kagera Sugar, 1-0 na Mbao, 3-0 na Toto Africans zote Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na 3-0 na Mwadui Uwanja wa Kambarage.
Rekodi hiyo ilivunjwa katika mchezo uliofuata Novemba 6, Simba SC ikilala 1-0 mbele ya African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kipa huyo mrefu akaenda kufungwa tena mabao mawili katika mechi iliyofuata tena Novemba 9 Wekundu wa Msimbazi wakipigwa 2-1 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Na hapo ndipo ‘wabaya wa Angban’ walipoanza kujitokeza wakimtoa kasoro kibao na kupendekezwa aachwe.
Kipa huyo wa zamani wa Chelsea FC ya England, alisajiliwa Simba SC msimu uliopita baada ya kufeli majaribio Azam FC, alikotua awali kujaribu bahati yake akashindwa kumvutia kocha Muingereza Stewart Hall aliyekuwa anaiongoza timu hiyo wakati huo.
Lakini mbele ya Muigereza mwingine, Dylan Kerr aliyekuwa anaifundisha Simba SC msimu uliopita, Angaban akafuzu majaribio na kusajiliwa. Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1985 mjini Anyama, alikuja Tanzania akitokea klabu ya Ligi Kuu ya kwao, Ivory Coast, Jeunesse.
Vincent Angban aliwahi kuchezea timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa mika 21 ingawa alikuwa amevuka umri huo katika harakati za kutafuta kusajiliwa The Blues, lakini pamoja na kuonyesha uwezo Stamford Bridge, haikuwa bahati yake jezi ya bluu.
Kipa huyo aliibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d'Anyama kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2005, ambako hata hivyo miaka miwili baadaye aliondoka na kwenda kujiunga na Sawe Sports msimu wa 2006/2007.
Mwaka 2007, Angban akajiunga na ASEC Mimosas ambako alikuwa kipa wa kwanza hadi mwanzoni mwa msimu wa 2009 alipoumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Yeboah.
Yeboah akawavutia zaidi makocha wa timu hiyo kwa ubora wake wa kuokoa michomo na akaendelea kudaka hata Angban alipopona.
Baada ya kumaliza Mkataba wake ASEC, Angban akarejea Jeunesse na baadaye akaenda London kudakia U21 ya Chelsea.
Amewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika michuano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha pia nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.
Amedakia pia timu ya taifa ya wakubwa ya Ivory Coast ‘Tembo’ katika michuano ya CHAN ikiwemo ile ya mwaka 2009 na ndiye aliyesimama langoni katika mechi na Tanzania, Taifa Stars ikishinda 1-0 bao pekee la Mrisho Ngassa.
Angban anaondoka Simba SC baada ya kudaka jumla ya mechi 56 na kufungwa mabao 25 huku mechi 34 akisimama langoni bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.

0 comments:
Post a Comment