// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HUKUMU YA KESSY; TFF YAAMURU YANGA IILIPE SIMBA MILIONI 50 NA FAINI JUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HUKUMU YA KESSY; TFF YAAMURU YANGA IILIPE SIMBA MILIONI 50 NA FAINI JUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 09, 2016

    HUKUMU YA KESSY; TFF YAAMURU YANGA IILIPE SIMBA MILIONI 50 NA FAINI JUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeitaka klabu ya Yanga kuilipa Simba SC Sh. Milioni 50,000 na faini ya Sh. Milioni 3 kwa kosa kumsajili beki Hassan Ramadhan Kessy kinyume cha utaratibu.
    "Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa,".  
    Taarifa ya Kamati imesema kwamba kwa mujibu wa kanuni za Ligi kifungu cha 69 (5), Yanga inapaswa kupewa adhabu itakayowafanya wanachama wote waheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na si kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda hadhi ya soka ya Tanzania. 
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro (katikati) akiwanua mikono wachezaji Hassan kessy (kushoto) na Juma Mahadhi (kulia)

    Aidha, Kamati imeagiza Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati, apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
    Na hiyo ni baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano na vielelezo na kubaini Kessy alikuwa na Mkataba na Simba uliokuwa unaisha Juni 15, mwaka 2016 na Yanga walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu nyingine.
    Kamati pia imesema TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Yanga SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Simba kama taratibu zinavyoelekeza. 
    "Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Yanga SC,".
    "Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba,".
    "Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima,"imesema barua ya Kamati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUKUMU YA KESSY; TFF YAAMURU YANGA IILIPE SIMBA MILIONI 50 NA FAINI JUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top