Na David Nyembe, MBEYA
YANGA SC imezinduka baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ushindi huo unaofuatia kipigo cha 2-1 kutoka kwa Mbeya City Jumatano, unawafanya mabingwa hao watetezi wapunguze idadi ya pointi wanazozidiwa na vinara wa Ligi Kuu, Simba SC hadi kubaki tano (35-30) baada ya timu zote kucheza mechi 14.
Wachezaji wa Yanga wakifurahia bao lililofungwa na Simon Msuva leo
Shujaa wa Yanga leo alikuwa ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu mwezi uliopita, Simon Happygod Msuva aliyefunga bao hilo pekee kwa penalti dakika ya 74 baada ya James Mwasote kumchezea rafu mshambuliaji Mzambia wa Yanga, Obrey Chirwa kwenye boksi.
Mapema dakika ya 55 Priosns walipoteza nafasi ya kufunga baada ya mkwaju wa penalti wa Lambert Sabiyanka kuokolewa na kipa wa Yanga, Benno Kakolanya. Penalti ilitokana na kiungo Kaseke kumchezea rafu Victor Hangaya ndani ya boksi.
Kikosi cha Prisons kilikuwa; Andrew Ntala, Benjamin Asukile, Salum Kimenya, Leonsi Mutalemwa, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambarti Sabiyanka, Mohemmed Samata, Victor Hangaya/ Meshack Selemani dk82 na Jeremiah Juma/Salum Bosco dk27.
Yanga; Beno Kakolanya, Mbuyu Twite, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan, Vicent Bossou, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Yussuf Mhilu/Simon Msuva dk46, Donald Ngoma, Obrey Chirwa/Matheo Anthony dk90 na Deus Kaseke/Amissi Tambwe dk56.

0 comments:
Post a Comment