SANAMU la mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic litawekwa mjini Stockholm, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Sweden (SvFF).
Sanamu hilo la heshima ambalo litawekwa nje ya Uwanja wa Friends Arena katika Jiji hilo la Sweden, linafuatia mshambuliaji huyo ngangari kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa nchi hiyo kwa miaka 10 mfululizo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 wa Manchester United, aliichezea Sweden mechi 114 na kuifungia mabao 62 kabla ya kustaafu baada ya Euro 2016.
Shirikisho la Soka la Sweden litatengeneza sanamu la gwiji wake, Zlatan Ibrahimovic
Mafanikio yake katika timu yanajumuisha mabao manne aliyofunga mwaka 2012 dhidi ya England katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja ambao sanamu lake litawekwa.
Ibrahimovic kwa sasa ameweka rekodi ya kushinda Mpira wa Dhahabu, mara 11 kwani tangu ianzishwe mwaka 1946 hakuna mchezaji ambaye ameshinda zaidi ya mara mbili na mchango wake huo unalipwa kwa ujenzi wa sanamu la ukubwa wa mita 2.7.
Akiipokea tuzo hiyo, Ibrahimovic alisema: "Inafikiriwa si sahihi. Wengi wanafikiri "Kwa nini yeye?" na mengine, lakini baada ya kazi yote ngumu kwa miaka 15 timu ya taifa na miaka 20 kwenye klabu, itafikiriwa nimeheshimiwa,".
"Kwa kawaida heshima kama hizi mtu hupata ukishakufa, lakini najisikia nipo hai. Nikifa, sanamu hili litaishi milele,"alisema.
0 comments:
Post a Comment