Na David Nyembe, MBEYA
KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kwamba refa Rajab Mrope wa Ruvuma alilikubali bao la pili la Mbeya City jana baada ya ushauri wa Kamanda wa Polisi Mbeya, Dhahiri Kidavashali.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo mjini Mbeya, Pluijm alisema kwamba halikuwa bao halali na refa alikwishalikataa awali, lakini kwa agizo la Kidavashali akalikubali.
“Bao la pili lilikuja baada ya mpira wa adhabu tena. Refa aliwarudisha nyuma wachezaji wetu na kuwaambia wasubiri filimbi na wakati huo huo bila filimbi ya refa wakapiga mpira wa adhabu na kufunga ikawa 2-0,”.
Pluijm amesema refa alilikubali bao la pili la Mbeya City jana baada ya ushauri wa Kamanda wa Polisi Mbeya, Dhahiri Kidavashali
“Wachezaji wetu walilalamikia lile bao na akakubali kwamba Mbeya City lazima warudie kupiga mpira ule. Mengi (vurugu) yakatokea kisha Kamanda wa Polisi Mbeya akawashauri marefa kulikubali lile bao,”alisema Pluijm.
Lakini Kivadashali amekana tuhuma za Pluijm akisema; “Sikumuamuru refa, nilichokifanya, baada ya mashabiki wa Mbeya City kuanza kutupa mawe uwanjani, niliwaamuru Polisii waende kuwadhibiti na kumlinda refa,”.
Na Kamanda huyo akasema kwamba anashukuru vijana wake walifanya kazi yao vizuri mchezo ulimalizika salama na kuhusu maamuzi ya marefa yeye hahusiki na hakuingilia.
Pluijm alisema bao lile lililokuja wakati timu yake inasaka bao la kusawazisha kufuatia Mbeya City kutangulia kwa bao la mapema dakika ya sita, liliwavunja nguvu vijana wake.
Mholanzi huyo amesema kwamba pamoja na ukweli huo, timu yake jana haikucheza vizuri kwa ujumla.
“Tulizungumza sana kabla ya mchezo, na niliwaonya (wachezaji) kuwa makini, hatukuuanza mchezo kwa umakini wa kutosha. Tukafungwa bao dakika ya sita kutokana na mpira wa adahbu baada ya makosa ya kipa Dida (Deo Munishi) ambaye alikuwa hajajipanga vizuri,”.
“Hii haikuisaidia timu pia kurudi mchezoni, ilikuwa siku mbaya sana kwetu. Hatukucheza mchezo wetu wa pasi,”alisema.
Yanga jana ilipoteza mechi ya pili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufungwa mabao 2-1 na
Mbeya City Council FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Kwa matokeo hayo, mabingwa watetezi, Yanga wanabaki na pointi zao 27 za mechi 13 na sasa wanazidiwa pointi nane na mahasimu, Simba SC wenye pointi 35 za mechi 13 pia.
Mabao ya MCC jana yalifungwa na Hassan Mwasapili dakika ya sita na Nahodha Kenny Ally dakika ya 36, wakati la Yanga lilifungwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 45 na ushei.

0 comments:
Post a Comment