// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OMOG ALUNDIKA VIUNGO WATANO MECHI NA LYON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OMOG ALUNDIKA VIUNGO WATANO MECHI NA LYON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, November 06, 2016

    OMOG ALUNDIKA VIUNGO WATANO MECHI NA LYON

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mcameroon, Joseph Marius Omog ameweka viungo watano na mshambuliaji mmoja tu leo kwenye mchezo dhidi ya African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Omog amemuanzisha Mrundi Laudit Mavugo pekee katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaoanza saa 10:00 jioni ya leo.
    Katika safu ya kiungo ‘amewalundika’ Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim, na Mwinyi Kazimoto. 
    Kocha Omog (kulia) ameweka viungo watano na mshambuliaji mmoja tu leo kwenye mchezo dhidi ya African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

    Kwa ujumla kikosi cha SImba leo ni; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim, Laudit Mavugo na Mwinyi Kazimoto. 
    Katika benchi wapo; Peter Manyika, Hamad Juma, Said Ndemla, Emmanuel Semwanza, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib na Mussa Ndusha. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OMOG ALUNDIKA VIUNGO WATANO MECHI NA LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top