Nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho hatafanyiwa upasuji kufuatia kuumia henka PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Liverpool imepata ahueni kufuatia habari kwamba nyota wake, Philippe Coutinho atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita tu.
Mkali huyo wa mabao anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu baada ya kuumia kwenye mechi na Sunderland, lakini bahati nzuri mambo si mabaya kama yalivyotarajiwa.
Vipimo vimeonyesha mchezaji huyo hahitaji kufanyiwa upasuaji na maana yake anaweza kurejea kwa ajili ya mchezo wa Liverpool na Manchester United katikati ya Januari.
Mechi zijazo za Liverpool zinatarajiwa kuwa changamoto nzuri kwa kocha Jurgen Klopp, akimenyana na majirani zake wa Merseyside, Everton na washindani wao wa taji, Manchester City. Ikiwa Coutinho atakuwa fiti kabla ya Januari 15, nyota huyo wa Brazil anaweza kuwamo kwenye safari ya Old Trafford kwa mechi dhidi ya kocha Jose Mourinho na mahasimu, Man United.
Coutinho aliumia hivi karibuni katika mchezo kati ya Liverpool na Sunderland, baada ya kugongwa na Didier N'dong.
0 comments:
Post a Comment