// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERIKALI YAWAAMBIA MANJI, DEWJI; "ANZISHENI TIMU ZENU KAMA BAKHRESA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERIKALI YAWAAMBIA MANJI, DEWJI; "ANZISHENI TIMU ZENU KAMA BAKHRESA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 26, 2016

    SERIKALI YAWAAMBIA MANJI, DEWJI; "ANZISHENI TIMU ZENU KAMA BAKHRESA"

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SERIKALI imewashauri wafanyabiashara vijana, Mohamed 'Mo' Dewji na Yussuf Manji kuanzisha timu za kama mfanyabishara mwenzao mwenye asili ya Kiasia agiza, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa kuliko kuzing'ang'ania Simba na Yanga.
    Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja alipozungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dart es Salaam kuhusu fukuto la mabadiliko Simba na Yanga.
    Kiganja kwanza ameagiza kusitishwa michakato yote inayoendelea ya kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa Wanachama kwenda katika umiliki wa hisa na ukodishwaji kwa Klabu za Simba na Yanga hadi kutakapofanyika marekebisho ya katiba zao.
    Amesema klabu hizo zinapaswa kurekebisha katiba zao kwanza kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9) .
    Kiganja alisema kuwa mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye Klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kupinga michakato hiyo kitu ambacho sio kizuri na pia sio ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.
    "Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa Wanachama kwenda kwa uwekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapo fanya mabadiliko kwa mujibu wa Katiba za Klabu zao," alisema Kiganja.
    Aidha BMT imemtaka mdau au mwanachama yoyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye Klabu hizo ni vema angeanzisha timu yake kama Saidi Salum Bakhresa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko kwavile timu hizo zina Wanachama wengi.
    Kiganja alisema kuwa michakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote kwani mabadiliko yoyote ndani ya klabu hizo lazima yafuate Katiba zao.
    Manji anataka kuikodisha Yanga kwa miaka 10, wakati Dewji anataka kununua asilimia 51 ya hisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAWAAMBIA MANJI, DEWJI; "ANZISHENI TIMU ZENU KAMA BAKHRESA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top