// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA DODOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA DODOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, October 24, 2016

    MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA DODOMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MFALME Mohammed VI wa Morocco amekubali kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu katika makao makuu ya nchi mjini Dodoma.
    Hayo yamesemwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla fupi ya kusaini makubaliano mbalimbali ya kibiashara kati ya Tanzania na Morocco iliyofanyika Ikulu mjini Dar es salaam.
    Akizungumza mbele ya Mfalme huyo ambaye alikuja nchini jana jioni, Rais Magufuli alisema kwamba alimuomba msaada wa kujenga Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu mjini Dodoma, ombi ambalo limekubaliwa.
    Rais Magufuli (kulia) akiwa na mgeni wake, Mfalme Mohamed V wa Morocco Ikulu mjini Dar es salaam

    Mfalme huyo aliwasili nchini nchini Oktoba 23, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Magufuli.
    Alitua Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam majira ya saa 11 Jioni na kupokewa na mwenyeji wake, Rais Magufuli kabla ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi la Jeshi la Wananchi Tanzania lililoandaliwa kwa heshima yake.
    Leo jioni Mfalme Mohammed VI atashiriki dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais Magufuli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top