NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi ameendelea kufurahua maisha ya soka baada ya kuteuliwa Mshambuliaji Bora wa Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga msimu uliopita.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoine Griezmann ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa La Liga katika sherehe zilizofanyika leo mjini Valencia.
Hata hivyo, sherehe hizo ziliingia doa kwa kususiwa na wachezaji Barcelona ambao hawakuhudhuria baada ya kukerwa kwa kitendo cha La Liga kutomuorodhesha kocha wao, Luis Enrique katika tuzo ya Kocha Bora.
Enrique hakuwamo hata katika orodha ya wawania tuzo licha ya kuiwezesha Barcelona kutwaa taji la La Liga.
Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya kiungo bora. Mshambuliaji wa Uruguay na Barcelona, Luis Suarez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora ea Dunia wa La Liga, wakati Atletico Madrid imetoa washindi wa tuzo za kocha Diego Simeone, Jan Oblak kipa bora na Diego Godin beki bora.
Ajabu mshambuliaji tegemeo wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo wa Ureno hajashinda tuzo yoyote.
0 comments:
Post a Comment