Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Kelvin Nashon Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada katika mazoezi ya timu hiyo jana kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Kongo. Serengeti Boys inajiandaa na mechi ya marudiano hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za U-17 Afrika mwakani Madagascar, baada ya kushinda 3-2 mchezo wa kwanza Dar es Salaam, Mchezo wa marudiano utafanyika Jumapili Uwanja wa Alphonse Massamba-Débat, Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, mjini Brazzaville PICHA ZOTE NA ALFRED LUCAS WA TFF
Wachezaji wa Serengeti Boys wakijifua jana Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo
Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada wakiwa mazoezini jana
Purukushani langoni ambako Dickson Job aliye hewani akikoa hatari langoni kwake
Kocha wa Makipa wa Serengeti Boys, Muharami Mohammed maarufu kwa jina la Shilton (wa pili kushoto) akiwanoa vijana wake, Kelvin Kayego (kushoto), Ramadhani Kabwili (wa tatu kushoto) na Samwel Brazio kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo.
Wachezaji wa Serengeti Boys wakijifua jana Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo
Madaktari wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Dk. Sheicky Mngazija (kushoto) na Gilbert Kigadye wakifuatilia kwa karibu mazoezi ya timu kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo.
0 comments:
Post a Comment