// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKWASA AMUWEKA BENCHI MWINYI MNGWALI, AMUANZISHA TSHABALALA STARS NA NIGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKWASA AMUWEKA BENCHI MWINYI MNGWALI, AMUANZISHA TSHABALALA STARS NA NIGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 03, 2016

    MKWASA AMUWEKA BENCHI MWINYI MNGWALI, AMUANZISHA TSHABALALA STARS NA NIGERIA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amemuweka benchi beki wa Yanga, Mwinyi Hajji Mngwali na kumuanziaha beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ upande wa kushoto katika mchezo dhidi ya Nigeria leo.
    Tanzania, au Taifa Stars ni wageni  wa Nigeria ‘Super Eagles’ jioni ya leo katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Gabon mwakani.   
    Na Mkwasa amewaanzisha Aishi Manula, Shomary Kapombe, Tshabalala, Andrew Vincent ‘Dante’, David Mwantika, Himid Mao, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, John Bocco, Mbwana Samatta na Simon Msuva.
    Mwinyi Mngwali anaanzia benchi leo mbele ya Tshabalala
    Katika benchi wapo Said Kipao, Mwinyi Mngwali, Ibrahim Rajab ‘Jeba’, Muzamil Yassin, Ibrahim Hajib, Farid Mussa na Juma Mahadhi.
    Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni kwa saa za Nigeri na SAaa 1:00 kwa saa za Tanzania Uwanja wa Uyo, Akwa Ibom.
    Taifa Stars na Super Eagles zote zimetupwa nje ya kinyang’anyiro cha tiketi ya Gabon mwakani, baada ya kuzidiwa kete na Misri waliofuzu kiulaini baada ya Chad kujitoa kwenye kundi hilo.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AMUWEKA BENCHI MWINYI MNGWALI, AMUANZISHA TSHABALALA STARS NA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top