Beki hodari wa kati wa Simba, Deo Njohole ‘OCD’ (wa pili kulia) akiwa na wachezaji wa Yanga wakati wa mapumziko katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes mwaka 1992 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam. Njohole alitokea kambi ya timu ya taifa, Jeshi la Wokovu kwenda kuchezea Yanga kama mchezaji mwalikwa baada ya kushawishiwa na wachezaji wa klabu hiyo aliokuwa nao kambini Taifa Stars. Wengine pichani ni Lawrence Mwalusako (kulia), Wastara Baribari (mbele kabisa), Ramadhani Kilambo (kushoto) na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ anayezungumza na Abbas Gulamali (sasa marehemu) aliyekuwa mfadhili wa klabu. Njohole hakuendelea kucheza Yanga baada ya mchezo huo.
UFC's Dana White: 'I Was Wrong,' Jake Paul 'Couldn't Do S--t' to Mike Tyson
in Fight
-
Mike Tyson lost decisively to Jake Paul on Friday night, but UFC president
Dana White thought Iron Mike proved something in the ring nonetheless.
During the…
19 minutes ago
0 comments:
Post a Comment