// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YATAHADHARISHA WACHEZAJI WATANO 'VIMEO' LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YATAHADHARISHA WACHEZAJI WATANO 'VIMEO' LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 22, 2016

    TFF YATAHADHARISHA WACHEZAJI WATANO 'VIMEO' LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitahadharisha klabu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wanamatatizo kwenye usajili wao.
    Klabu hizo ni pamoja na Majimaji ya Songea ambayo ina mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
    Mwadui FC ya Shinyanga; Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji huyo.
    Mbeya City ya Mbeya; Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba na Tanzania Prisons ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.
    African Lyon ya Dar es Salaam; Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
    Mbao FC ya Mwanza; Mchezaji Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27, 2016. Mbao FC isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YATAHADHARISHA WACHEZAJI WATANO 'VIMEO' LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top