// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IVORY COAST YAWASILI DAR KUIVAA TANZANIA SOKA LA UFUKWENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IVORY COAST YAWASILI DAR KUIVAA TANZANIA SOKA LA UFUKWENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 23, 2016

    IVORY COAST YAWASILI DAR KUIVAA TANZANIA SOKA LA UFUKWENI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Ivory Coast, imeingia Dar es Salaam, Tanzania leo saa 8.00 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea jijini Abidjan.
    Timu hiyo imekuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu wa ufukweni ambako itacheza na wenyeji Tanzania Ijumaa wiki hii kwenye uwanja maalumu ulioandaliwa kwa ajili ya mchezo huo.
    Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.

    Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, zitarudiana tena Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
    Kwa upande wa Tanzania, Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu, anaendelea na mazoezi na wachezaji wake 16 aliowatangaza wiki iliyopita. Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
    Wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahmad, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.
    Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST YAWASILI DAR KUIVAA TANZANIA SOKA LA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top