MAKUNDI YOTE LIGI YA MABINGWA ULAYA
Kundi A; Arsenal PSG, Basle na Ludogorets
Kundi B; Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas
Kundi C; Barcelona, Man City, Borussia Monchengladbach na Celtic
Kundi D; Bayern Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov
Kundi E; CSKA Moscow, Bayer Leverkusen, Tottenham na
Monaco
Kundi F; Real Madrid, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon na Legia Warsaw
Kundi G; Leicester, Porto, Club Bruges na Copenhagen
Kundi H; Juventus, Sevilla, Lyon na Dinamo Zagreb
Kocha mpya wa Manchester City, Pep Guardiola amepangwa na timu yake ya zamani, Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA Pep Guardiola atakutana Barcelona baada ya timu yake mpya, Manchester City kupangwa kundi moja na timu yake hiyo ya zamani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pep aliyetwaa taji hilo mara mbili akiwa na Barca, ameiwezesha City kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuitoa Steaua Bucharest katika mchujo.
Timu hizo mbili zimepangwa pamoja katika Kundi C dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na mabingwa wa Scotland, Celtic.
Katika droo iliyopangwa leo, Arsenal imewekwa Kundi A pamoja na Paris Saint-Germain, Basle na Ludogorets wakati Kundi B kuna Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas.Kundi D kuna Bayern Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov, Kundi E kuna CSKA Moscow, Bayer Leverkusen, Tottenham na Monaco, Kundi F kuna Real Madrid, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon na Legia Warsaw.
Kundi G kjuna Leicester City, Porto, Club Bruges na Copenhagen, Kundi H kuna Juventus, Sevilla, Lyon na Dinamo Zagreb.
0 comments:
Post a Comment