Na Mwandishi Wetu, SEKONDI
YANGA wameshituka kumuona Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba katika mazoezi yao Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi jioni ya leo.
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho leo kabla ya kumenyana na wenyeji Medeama FC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja huo wa Essipong Sports kesho jioni.
Na viongozi wa Yanga walioambatana na timu walishituka kumuona mtu ambaye walijiridhisha kabisa ni Kawemba, Mtendaji Mkuu wa Azam, FC akiwa anazungumza na viongozi wa Medeama.
Mtu anayedaiwa kuwa Ni Saad kawemba (katikati) akizungumza na Mghana leo Uwanja wa Essipong Sports
Mtu anayedaiwa kuwa ni Kawemba akiwa ametulia kwenye kiti na mwenyeji wake wa Ghana leo Uwanja wa Essipong, wakati Yanga na Medeama zikifanya mazoezi
Hata hivyo, kwa mujibu wa habari za ndani kutoka Azam FC, ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imezipata ni kwamba Kawemba amekwenda huko kushughulikia mpango wa Azam TV kuonyesha moja kwa moja mechi hiyo kesho.
"Kawemba amekwenda kwa ajili ya mambo ya Azam TV, na ameagizwa yeye kwa sababu anafahamiana na viongozi wengi wa mpira, si unajua yule alikuwa TFF,"kimesema chanzo.
Yanga ambayo jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya Bohar mjini hapa, siku moja baada ya kuwasili hapa, usiku wa Jumamosi kutoka Dar es Salaam imepania kushinda kesho ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Mchezo Hao utachezeshwa naRedouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou watakaoshika vibendera.
TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria Juamatno mjini Lubumbashi katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.
Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.

0 comments:
Post a Comment