Na Mwandishi Wetu, MBEYA
MBEYA City imezidi kujiimarisha kuelekea msimu ujao, baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo Daktari Ayoub Idrisa Semtawa kutoka Coastal Union iliyoshuka daraja.
Ayoub anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Mbeya City wiki hii, baada ya mwanzoni mwa wiki kusajiliwa beki wa Yanga, Rajab Zahir aliyekuwa anacheza kwa mkopo Stand United.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Ayoub aliyehitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), alisema kwamba baada ya kutua Mbeya City anataka kuongeza bidii ili autambulishe zaidi uwezo wake.
Dk Ayoub Idrisa Semtawa katika picha mbili tofauti, kulia akiwa ameshika jezi ya Mbeya City na kushoto akisaini Mkataba
“Coastal Union hatukuwa na msimu mzuri kwa ujumla, matatizo ya kiuongozi yalichangia sana, lakini sasa baada ya kusaini Mbeya City, natarajia kujipanga ili nifaney vizuri,”alisema.
Ayoub alizaliwa Julai 27, mwaka 1994 wilayani Muheza mkoani Tanga na alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Maendeleo, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.
Baadaye Ayoub alijiunga na sekondari ya Magila, iliyopo Muheza mkoani Tanga alikosoma hadi KIdato cha Nne, kabla ya kuhamia Muheza High School alikosoma hadi Kidato cha Sita.
Alijiunga na timu ya vijana ya U20 ya Coastal mwaka 2012 baada ya kuchezea timu za mtaani kama Vagarant ya Kilombero, Fish Stars na Bambino za Muheza.
Alikuwemo katika kikosi cha Coastal kilichofika fainali ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati ya vijana mwaka 2012 iliyofanyika Burundi pamoja na kikosi kilichofika Fainali ya Kombe la Uhai mwaka juzi na kufungwa na Azam, kabla ya mwaka uliofuata kuwafunga Yanga na kutwaa ubingwa.

0 comments:
Post a Comment