// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
KASEKE AANZA MAZOEZI YANGA SC IKIJIFUA JANGWANI MARA YA KWANZA CHINI YA MANJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEKASEKE AANZA MAZOEZI YANGA SC IKIJIFUA JANGWANI MARA YA KWANZA CHINI YA MANJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
KASEKE AANZA MAZOEZI YANGA SC IKIJIFUA JANGWANI MARA YA KWANZA CHINI YA MANJI
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO Deus David Kaseke jana amefanya mazoezi na Yanga baada ya kukosekana kwa wiki tatu kutokana na maumivu aliyopata baada ya ajali ya pikipiki. Kaseke alikosekana Yanga SC katika mechi zote dhidi ya Medeama ya Ghana Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, wakitoa sare ya 1-1 nyumbani Dar es Salaam na kufungwa 3-1 Ghana baada ya ajali ya pikipiki. Lakini sasa kiungo huyo amepona majeraha yake naa anajaribu kurejea kwa ajili ya mchezo ujao Agosti 13 dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha Hans van der Pluijm akizungumza na kiungo Deus Kaseke mazoezini jana Jangwani
Wachezaji wa Yanga wakinywa maji wakati wa mapumziko mafupi jana
Yanga jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wake wa Kaunda, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam baada ya muda mrefu na labda kwa mara ya kwanza kabisa, tangu Yussuf Manji awe Mwenyekiti. Na kocha Mholanzi Hans van der Pluijm alilazimika kushuka Jangwani baada ya jitihada za kupata uwanja wa kukodi kama ilivyo ada yao kugonga mwamba jana. Yanga ilirejea Dar es Salaam Alhamisi usiku ikitokea Ghana ambako Jumanne ilipigwa 3-1 Medeama katika mfululizo wa mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho. Na hicho kilikuwa kipigo cha tatu katika mechi nne, baada ya awali kufungwa 1-0 mara mbili nyumbani na ugenini, dhidi ya MO Bejaia Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam.
Beki Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou akipasha jana
Hassan Kessy naye ameendelea na mazoezi ingawa hawezi kucheza mashindano haya
TP Mazembe ndiyo wanaongoza kundi hilo kwa pointi zao 10 baada ya kushinda mechi tatu na sare moja, wakifuatiwa na Bejaia na Medeama ambao kila mmoja ana pointi tano wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
-
TP Mazembe have won the 2024 CAF Women’s Champions League title after they
defeated ASFAR 1-0 in the final on Saturday evening, played at the Ben
M’Hamed...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment