Gonzalo Higuain amejiunga na Juventus kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 76 kutoka Napoli PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Juventus imemsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 76 kutoka Napoli, zote za Italia.
Ada ya uhamisho italipwa kwa awamu mbili, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umrin wa miaka 28 atalipwa mshahara wa Pauni Milioni 6.3 kwa mwaka baada ya kodi.
Taarifa ya Juventus imesema; "Juventus Football Club leo inaweza kuthibitisha imemsajili Gonzalo Higuain kwa dau la Euro Milioni 90, zitakazolipwa kwa awamu mbili ndani ya miaka miwili. Mchezaji huyo amesaini Mkataba wa miata mitano,". Na kwa usajili huo, Higuain anaingia kwenye orodha ya wachezaji ghali kuwahi kusajiliwa duniani.
Orodha hiyo inaongozwa na Gareth Bale aaliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86 mwaka 2013 kutoka Tottenham kwenda Real Madrid, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyesajiliwa kwa Puni Milioni 80 mwaka 2009 kutoka Manchester United kwenda Real Madrid.
Wengine ni Neymar aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 71.5 mwaka 2013 kutoka Santos kwenda Barcelona, Luis Suarez aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 65 mwaka 2014 kutoka Liverpool kwenda Barcelona na James Rodriguez aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 63 mwaka 2014 kutoka Monaco kwenda Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment