Nyota wa Ujerumani, Shkodran Mustafi (kulia) akishangilia na wachezaji wenzake, Sami Khedira (Namba 6) na Jerome Boateng (Namba 17) baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 19 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine Uwanja wa Stade Pierre-Mauroy mjini Villeneuve d'Ascq kwenye mchezo wa Kundi C Euro 2016. Bao la pili la Ujerumani limefungwa na Bastian Schweinsteiger dakika ya 90 na ushei PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Gareth McAuley (kushoto) akipambana na mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski katika mchezo wa Kundi C Euro 2016 leo Uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice, Ufaransa. Poland imeshinda 1-0, bao pekee la Arkadiusz Milik PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment