Na Mwandishi Wetu, BEJAIA
KOCHA Mholanzi, Hans van der Pluijm hajamhusisha kabisa beki Hassan Ramadhani Kessy katika mchezo wa leo dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia.
Na si Kessy tu, Pluijm hajamhusisha mchezaji yeyote kati ya watano wapya aliosajili wengine wakiwa kipa Benno Kakolanya, beki Andrew Vincent na viungo Juma Mahadhi na Mzambia Obrey Chirwa.
Hiyo inafuatia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuomba barua ya Kessy kuruhusiwa na klabu yake ya zamani, Simba SC kuhamia Yanga.
Rasmi Mkataba wa Kessy unamalizika mwezi huu na ili aanze kuichezea Yanga anatakiwa kuwa na barua ya kuruhusiwa kuondoka na Simba.
Pluijm alimtegemea Kessy kuziba pengo la majeruhi Juma Abdul, ambaye amebaki Dar es Salaam na amempanga Mbuyu Twite beki ya kulia.
Kikosi kamili cha Yanga kinachoanza ni; Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Junior Twite, Oscar Fanuel Joshua, Kelvin Patrick Yondani 'Cotton', Vicent Bossou, Thabani Michael Kamusoko, Simon Happygod Msuva, Harouna Fadhil Niyonzima, Donald Dombo Ngoma na Amiss Jocelyn Tambwe Deus David Kaseke.
Katika benchi wapo; Ally Mustafa Mtinge 'Bathez', Mwinyi Haji Ngwali, Pato George Ngonyani, Antony Simon Matheo, Juma Said Makapu na Godfrey Furaha Mwashiuya.
Televisheni ya Algeria pekee ndiyo itakayoonyesha mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 4:00 usiku kwa Saa za Algeria na Saa 6:00 usiku kwa Saa za Tanzania.

Kessy wa pili kulia amepandishwa jukwaani Yanga ikimenyana na MO Bejaia |

0 comments:
Post a Comment