KLABU ya Manchester United ya England imeanza majadiliano na Juventus ya Italia juu ya kiungo kumsajili tena kiungo wake wa zamani, Mfaransa Paul Pogba.
Kwa mujibu wa gazeti la L'Equipe la Ufaransa, Pogba, mwenye umri wa miaka 23 sasa, aliyeondoka Man United kuhamia Juventus kama mchezaji huru mwaka 2012 baada ya kukataa kuongeza Mkataba chini ya kocha Sir Alex Ferguson kutokana na kutopewa nafasi ya kucheza, sasa anaweza kurejea Old Trafford.
Paul Pogba anaweza kurejea Manchester United akiwa na umri wa miaka 23 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Chini ya Ferguson, Pogba alicheza mechi saba tu za kikosi cha kwanza Man United, lakini sasa chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho Mashetano hao Wekundu wanataka kumrejesha Old Trafford.
Na inasemekana Juve, maarufu kama Kibibi Kizee cha Turin haiwezi kumuuza nyota wake huyo kwa dau la chini ya Pauni Milioni 82.8..
L'Equipe limesema kwamba , kocha mpya wa Man United, Jose Mourinho anataka kutambulisha mfumo wa 4-3-3 msimu ujao na anamtaka Pogba akachezea pamoja na Nahodha Wayne Rooney katika safu ya kiungo katikati, pamoja na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial na Henrikh Mkhitaryan pembeni.
0 comments:
Post a Comment