// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FELA NA WANAWE WAWAFARIJI WAGONJWA HOSPTALI YA TEMEKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FELA NA WANAWE WAWAFARIJI WAGONJWA HOSPTALI YA TEMEKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 26, 2016

    FELA NA WANAWE WAWAFARIJI WAGONJWA HOSPTALI YA TEMEKE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KITUO cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe, kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wagongwa waliolazwa katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
    Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho leo asubuhi, Said Fella, alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
    Alisema kuwa alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.

    Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanaye, Said Fella akizungumza katika hospitali ya Temeke leo

    “Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema Fella.
    Akipokea msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.
    “Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oxymeter cha kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka au la na Mashine ya Nebulizer  yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema Nyumbiage.
    Akizungumza kwa niaba ya wenzake takribani 50 alioambatana nao hospitalini hapo, msanii anayeunda kundi la Yamoto, Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya hivyo wakati mwingine watakapopata nafasi.
    Fela akikabidhi misaada hiyo leo hospitali ya Temeke mjini Dar es Salaam
    Wasanii wa kikundi cha Mkubwa na Wanawe wakiwafariji wagonjwa wadini 
    Wagonjwa wamefarijika na ziara ya kikundi cha Mkubwa na Wanawe leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FELA NA WANAWE WAWAFARIJI WAGONJWA HOSPTALI YA TEMEKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top