Beki wa kulia wa Brazil, Dani Alves atahitimisha miaka yake ya nane ya kucheza Barcelona msimu huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Barcelona imethibitisha Dani Alves ataondoka, lakini imekana kuwa na mpango wa kumchukua Hector Bellerin wa Arsenal akazibe pengo lake.
Alves amekuwa kazini Nou Camp tangu asalijiwe kutoka Sevilla miaka nane iliyopita.
Mkurugenzi wa Usajili, Roberto Fernandez amesema: "Dani ameamua kuondoka na tunapaswa kukubali uamuzi wake. Ameithibitishia klabu anachotaka ni kuondoka.
"Tunapaswa kukumbuka kwamba amemaliza Mkataba wake mwaka uliopita, lakini hatukuweza kusajili mchezaji yeyote kwa sababu ya adhabu ya kufungiwa kusajili na FIFA na hivyo yalikuwa mazingira magumu kwetu na akaongeza Mkataba. Lakini sasa anatafuta mazingira mazuri zaidi kwake,".
Alves amekaribia kumalizana na Juventus na wakala wake, Dinorah Santana pia anafanya mazungumzo na Paris Saint-Germain.
Beki huyo wa kulia anaweza kupewa dau zuri kwa sababu katika Mkataba wake mpya, kwa sababu wakati anaongeza Mkataba Barca mwaka jana, walikubaliana vigogo hao wa Hispania hawatapa ada ya uhamisho akiondoka Camp Npu.
Mkongwe huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 33, anaondoka Barca baada ya miaka nane, akishinda mataji 23.
0 comments:
Post a Comment