TIMU ya taifa ya Algeria imejihakikishia kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Gabon kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ugenini jana dhidi ya Shelisheli Uwanja wa Stade Linite.
Mechi hiyo ilipewa jina ‘Daudi na Goliath’ kutokana na Algeria kuwa timu inayoongoza kwa ubora wa soka barani na Shelisheli wanashika nafasi ya 51.
Mabao ya Algeria yamefungwa na nyota wa Lille ya Ufaransa, Yassine Benzia dakika ya 40 kabla ya kutoka dakika ya 56 kufuatia kuumia na pili akafunga El Arabi Hilal Soudani akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ryad Boudebouz ambaye alichezewa rafu na Nelson Laurence.
Wenyeji walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga mwishoni mwa mchezo kupitia kwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Shelishelir, Carl Hall na Dean Suzette.
Kwa ushindi huo, Algeria inafikisga pointi 13 katika Kundi J na moja kwa moja kufuzu AFCON, ikifuatiwa na Ethiopia yenye pointi tano, wakati Shelisheli na Lesotho kila moja ina pointi nne.
Algeria inaungana na Morocco kuwa timu pekee zilizojihakikishia tiketi ya fainali za AFCON ya mwakani, ukiondoa wenyeji Gabon.

Algeria imeungana na Morocco kufuzu Fainali za AFCON mwakani |
Kwa ushindi huo, Algeria inafikisga pointi 13 katika Kundi J na moja kwa moja kufuzu AFCON, ikifuatiwa na Ethiopia yenye pointi tano, wakati Shelisheli na Lesotho kila moja ina pointi nne.
Algeria inaungana na Morocco kuwa timu pekee zilizojihakikishia tiketi ya fainali za AFCON ya mwakani, ukiondoa wenyeji Gabon.
0 comments:
Post a Comment