BEKI wa Liverpool, Mamadou Sakho katika mazingira ya kustaajabisha ameruhusiwa kuichezea Ufaransa kwenye Fainali za Euro 2016 baada ya UEFA kuamua kusitisha kwa muda adhabu ya kufungiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps sasa ana saa 72 za kuamua kumjumuisha Sakho kwenye kikosi chake au kufuatia kuumia kwa Raphael Varane wa Real Madrid.
Vikosi vyote vya Euro 2016 vinatakiwa kuwa vimewasilishwa hadi kufika Mei 31, ingawa kujumuishwa kwa Sakho kutazua utata baada ya kugundulika kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni Machi 17.
Mamadou Sakho ameruhusiwa kuichezea Ufaransa katika Euro 2016 baada ya UEFA kusitisha adhabu yake ya kutumia dawa za kulevya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Awali Sakho alifungiwa siku 30 Aprili 28 kufuatia vipimo alivyofanyiwa baada ya mchezo wa Europa League dhidi ya Manchester United kuthibitisha alitumia dawa hizo.
Adhabu hiyo inamalizika Jumamosi na UEFA imeshindwa kupiga hatua zaidi baada ya Sakho kuwasilisha utetezi wake Jumatatu.
Timu ya utetezi wa Sakho iliwasilisha vielelezo vya kisayansi katika kesi hiyo na UEFA imeiagiza Kamati yake Nidhamu kwanza kuchunguza zaidi kabla ya hatua kuchukuliwa.
Na baada ya adhabu yake ya awali kusitishwa, kwa sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, Sakho anaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha Les Bleus.
0 comments:
Post a Comment