MSHAMBULIAJI kinda wa Manchester United, Marcus Rashford nyota yake imeendelea kung'ara baada ya kuitwa katika kikosi ncha awali cha England cha wachezaji 26 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016.
Kinda huyo wa umri wa miaka 18, Rashford, ambaye alichezea kikosi cha kwanza cha Man United Februari mwaka huu, ni kati ya washambuliaji watano walioitwa na kocha Roy Hodgson jana.
England itacheza mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya Uturuki, Australia na Ureno kabla ya kwenda Ufaransa kwenye Euro.
Winga Andros Townsend naye ameitwa baada ya kumalizia vizuri Ligi Kuu ya England akiwa na Newcastle United iliyoteremka daraja.
Mshambuliaji chipukiiz wa Manchester United, Marcus Rashford amejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha England kwa ajili ya Euro 2016
0 comments:
Post a Comment