TIMU ya Manchester United imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 3-1 usiku huu dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford leo, ilikuwa ufanyike juzi lakini ukaahirishwa kutokana na hofu kutegwa kwenye Uwanja huo.
Nahodha Wayne Rooney aliifungia United bao la kwanza akimalizia krosi ya Anthony Martial dakika ya , hilo likiwa bao lake la 100 kufunga Uwanja wa Old Trafford.
Nahodha wa Man United, Wayne Rooney akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuiwezesha timu yao kufuzu Europa League kwa kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Marcus Rashford, akicheza mechi yake ya kwanza baada ya kuitwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya michuano ya Euro 2016, akaifungia United bao la pili dakika ya .
Winga Ashley Young aliyetokea benchi akaifungia United bao la tatu dakika ya akimalizia pasi ya Nahodha Rooney na kumalizia msimu kimtindo.
Kipa David de Gea akanyimwa tuzo ya "Glavu za Dhahabu' baada ya kutunguliwa na beki wake, Chris Smalling aliyejifunga dakika ya mwisho.
Man United inafikisha pointi 66 kwa matokeo hayo, baada ya kucheza mechi 38 ikiwa katika nafasi ya tano, mbele ya Southampton yenye 63 za mechi 38 pia.
Leicester City ndiyo mabingwa wapya wa England baada ya kumaliza na pointi 81 za mechi 38, wakifuatiwa na Arsenal wenye pointi 71, Tottenham Hotspur pointi 70 na Manchester City pointi 66, wakiwazidi kwa wastani wa mabao mahasimu wao, Man United.

0 comments:
Post a Comment