Beki wa Coastal Union, Miraj Adam (kushoto) akigeuka na mpira baada ya kumzidi maarifa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (kulia) katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mechi hiyo ilivunjika dakika ya 110 kati ya 120 baada ya mashabiki kumjeruhi mshika kibendera namba mbili, Charles Simon wa Dodoma, Yanga ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1
![]() |
Beki wa Coastal Union, Hamad Juma akimtoka kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima |
![]() |
Viungo Mcameroon wa Coastal Union, Youssouf Sabo (kushoto) na Mnyarwanda Haruna Niyonzima wa Yanga kulia wakipambana |
![]() |
Beki wa Yanga, Oscar Joshua (kushoto) akimtoka kiungo wa Coastal Union, Youssouf Sabo |
![]() |
Kikosi cha Yanga leo Uwanja wa Mkwakwani kabla ya mchezo huo |
![]() |
Kikosi cha Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya mchezo na Yanga |
0 comments:
Post a Comment