// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, April 09, 2016

    WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO

    Issoufou Boubacar anaanza leo katika mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri leo

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluim amemuanzisha kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar katika mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri leo.
    Yanga inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10:00 jioni ya leo kumenyana na Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 19 mjini Cairo.
    Na Pluijm amefanya marekebusho madogo kutoka kikosi chake maarufu kilichokuwa kikicheza mechi za hivi karibuni.
    Kiungo Salume Telela amechukua nafasi ya Pato Ngonyani pale chini na winga Issoufou Boubacar amechukua nafasi ya Simon Msuva upande wa kushoto wa Uwanja.
    Safu ya ulinzi ya Yanga inaendelea kuwa vile vile ikiundwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, beki wa kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Mngwali, katikati Vincent Bossou na Kevin Yondan. 
    Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Salum Telela, Deusi Kaseke, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Issoufou Boubacar.
    Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Paul Nonga, Godfrey Mwashuya na Simon Msuva.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top