IDADI ya timu za kufuzu Fainali za 10 za Kombe la Mataifa ya Afrika 2016 kwa wanawake imekamilika.
Mabingwa watetezi Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, Kenya zilijihakikishia nafasi zao juzi zikiungana na Misri, Equatorial Guinea na Zimbabwe ambazo zilifuzu mapema.
Katimu timu zote zilizofuzu, Kenya ndiyo imestaajabisha kwa kufuzu mara ya kwanza kwenye michuano hiyo tangu ianze mwaka 1998.
Timu hiyo maarufu kwa jina la utani Harambee Starlets imefuzu baada ya kuitoa Algeria, kufuatia sare ya 1-1 mjini Nairobi na sare ya 2-2 ugenini hivyo kufuzu kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3. Mkongwe Naima Bouhenni aliifungia Algeria bao la kuongoza dakika ya 23, kabla ya Cheris kuwasawazishia wenyeji dakika ya 74.
Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika katika miji ya Yaounde na Limbe, Cameroon kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 3.

Wachezaji wa Kenya wakifurahia baada ya kuitoa Algeria juzi |
Timu hiyo maarufu kwa jina la utani Harambee Starlets imefuzu baada ya kuitoa Algeria, kufuatia sare ya 1-1 mjini Nairobi na sare ya 2-2 ugenini hivyo kufuzu kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3. Mkongwe Naima Bouhenni aliifungia Algeria bao la kuongoza dakika ya 23, kabla ya Cheris kuwasawazishia wenyeji dakika ya 74.
Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika katika miji ya Yaounde na Limbe, Cameroon kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 3.
0 comments:
Post a Comment