// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HIVI NDIVYO KILIVYONUKA JANA MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HIVI NDIVYO KILIVYONUKA JANA MKWAKWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 25, 2016

    HIVI NDIVYO KILIVYONUKA JANA MKWAKWANI

    Beki wa Yanga, Mtogo Vincent bossou 'akianua' mpira mbele ya mshambuliaji wa Coastal Union, Ally Ahmed 'Shiboli' jana katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mechi hiyo ya dakika 120 ilivunjika dakika ya 110 wakati Yanga inaongoza 2-1 baada ya mashabiki kumjeruhi mwa mawe mshika kibendera namba moja, Charles Simon wa Dodoma
    Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke (kushoto) akimtoka kiungo wa Coastal Union, Juma Mahadhi
    Beki wa Yanga, Juma Abdul akiruka miguu ya beki wa Coastal Union, Adeyoum Ahmed
    Beki wa Yanga, Kevin Yondan aliyecheza kama kiungo wa ulinzi jana akimdhibiti kiungo wa Coastal, Juma Mahadhi
    Nahodha wa Coastal na kiungo Abdulhalim Humud akiinua mguu mbele ya kiungo wa Yanga, Deus Kaseke
    Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimdhibiti kiungo Mcameroon wa Coastal, Youssouf Sabo (kulia)
    Kiungo wa Coastal, Ismail Mohammed (kushoto) akiwania mpira wa juu na beki wa Yanga, Vincent Bossou
    Kiungo wa Coastal, Youssouf Sabo akiondoka na mpira mbele ya kiungo wa Yanga, mzimbabwe Thabani Kamusoko 
    Beki wa Coastal Union, Mbwana Khamis 'Kibacha' (katikati) akipiga wa juu kwa staili ya aina yake katikati ya wachezaji wa Yanga, Kamusoko kulia na winga Simon Msuva (kushoto)
    Beki wa Yanga Kevin Yondan akifanya vitu vyake jana kama kiungo wa ulinzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIVI NDIVYO KILIVYONUKA JANA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top