Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bin Slum Tyres Limited, Nassor Bin Slum (katikati) akionyesha kitambaa chekundu kumpigia huku akipiga yowe kumuambia refa wa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ampe kadi nyekundu beki wa Yanga, Oscar Joshua baada ya kumpiga beki wa Coastal Hamad Juma jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Bin Slum ambaye ni mwanachama wa Coastal hakufurahishwa na uchezeshaji wa marefa wa mchezo huo uliovunjika dakika ya 110 Yanga ikiwa inaongoza 2-1 baada ya mashabiki kumpiga jiwe mshika kibendera namba moja
Refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga (kushoto) akisikiliza utetezi wa winga wa Yanga, Simon Msuva kwa mchezaji mwenzake, Oscar Joshua (wa pili kulia). Kulia ni Hamad Juma wa Coastal akisikilizia maamuzi ya refa, ambaye mwishowe akatoa kadi ya njano. Picha ya chini Oscar akiwa amejishika uso baada ya kupigwa ngumi na Hamad Juma. Oscar alimrudishia Hamad hapo kwa hapo, tukio ambalo Bin Slum alilitafsiri ni la kadi nyekundu
|
0 comments:
Post a Comment