AZAM FC WAACHA NDEGE, WAPANDA NDEGE KUIFUATA MWADUI, YANGA SAFARI TANGA
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM AZAM FC imerejea mjini Dar es Salaam jioni ya leo kutoka Tunisa ambako Jumanne ilifungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance na kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika. Azam FC iliondoka Tunis jana mchana ikipitia Dubai, baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 na Esperance kufuatia kushinda 2-1 Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Na mara baada ya kuwasili, Azam FC itaunganisha ndege nyingine baadaye Saa 1:45 usiku kuelekea mjini Mwanza, ambako watalala kabla ya kesho asubuhi kuanza safari ya barabara kwenda Mwadui mkoani Shinyanga.
Viungo Himid Mao (mbele) na Jean Baaptiste Mugiraneza wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo
Kushoto ni beki Erasto Nyoni anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia
Azam FC Jumapili wanatarajiwa kucheza na wenyeji Mwadui katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC). Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo itachewa Tanga Jumapili pia kati ya Yanga SC na wenyeji Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani. Yanga nayo imerejea leo kutoka Misri, ambako juzi ilifungwa 2-1 na wenyeji Al Ahly katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam. Hata hivyo, Yanga sasa itamenyana na Sagrada Esperanca ya Angola kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam kati ya Mei 6 na 8 na marudiano ugenini kati ya mei 17 na 18. Yanga SC leo watalala katika hoteli ya Valley View, Kariakoo, Dar es Salaam na asubuhi mapema kesho watasafiri kwa basi lao kwenda Tanga.
Kutoka kulia Salum Abubakar, Kipre Balou na Allan Wanga wakiwasili JNIA leo
Ramadhani Singano 'Messi' mbele wakati wa kuwasili JNIA
Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad (kushoto) akiwaongoza viongopzi wenzake baada ya kutoka JNIA
Samuel Eto’o eyes CAF Exco seat
-
Cameroonian Football Football (FECAFOOT) president Samuel Eto’o is keen to
become a member of the Confederation of African Football (CAF)’s executive
com...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment