// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAZIRI MKUU MGENI RASMI, KIINGILIO STARS V CHAD BUKU TANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAZIRI MKUU MGENI RASMI, KIINGILIO STARS V CHAD BUKU TANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 26, 2016

    WAZIRI MKUU MGENI RASMI, KIINGILIO STARS V CHAD BUKU TANO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa (pichani kushoto) kwa kubali kuwa mgeni rasmi katika mchezo kati ya Tanzania v Chad utakaochezwa siku ya Jumatatu Dar es salaam.
    Malinzi pia amemshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa kufanikisha ujio wa Waziri Mkuu kwa kufuatilia kwa karibu maombi ya TFF ya Machi 21, mwaka huu kumuomba Waziri Mkuu awe mgeni rasmi katika mchezo huo.
    Na TFF leo limetaja viingilio vya mchezo wa huo kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kundi G siku ya Jumatatu, bei ya chini ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.
    Viingilio vya mchezo huo vimegawanyika katika makundi matatu, ambapo kiingilio cha juu kitakua shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa VIP A, na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa VIP B, na kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na orange itakua shiligi elfu tano (5,000).
    Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Jumapili saa 2 asubuhi katika vituo vinne ambavyo ni kituo cha mafuta Buguruni (Buguruni), Ubungo Oilcom (Ubungo) na Dar Live (Mbagala), na Jumatatu tiketi zitauzwa katika viunga vya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Kwa upande wa Taifa Stars iliyoweka kambi katika hoteli ya Urban Rose inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Chad.
    Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Djibouti wanatarajiwa kuwaisli leo jioni ambao ni mwamuzi wa kati Djamel Aden Abdi, Abdilahi Mahamoud, Farhan Bogoreh Salim, Farah Aden Ali, huku kamisaa wa mchezo akiwa Andrea Abdallah Dimbiti kutoka nchini Sudan Kusini.
    Wakati huo huo: TFF limeomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Johann Cruffy aliyefariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa Saratani.
    Katika taarifa aliyoituma kwa Rais wa Chama cha Soka cha Uholanzi, Rais wa TFF Jamal Malinzi amemwelezea Marehemu Cruyff kama gwiji aliyetoa mchango mkubwa kama mchezaji na kocha katika timu ya Taifa ya nchi yake na klabu za Barcelona, Ajax, Lavanet mwaka 1964 – 1977.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI MKUU MGENI RASMI, KIINGILIO STARS V CHAD BUKU TANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top