// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 28, 2016

    SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda (FUFA) kaufuatia kifo cha mlinda mlango Abel Dhaira kilichotokea jana jijini Kampla.
    Katika salamu hizo za rambirambi, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki, FUFA kufuatia msiba Dhaira, na kusema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hiki cha maombelezo.
    Dhaira alifariki jana Jumapili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa Kansa
    Wakati wa uhai wake Dhaira aliwahi kuidakia timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na kuvichezea vilabu vya Express FC, URA (Uganda), AS Vita (Congo DR), Simba SC (Tanzania) na klabu ya BV Vestmannaeyjar ya Iceland.
    Abbel Dhaira (kushoto) siku za mwisho za uhai wake nchini Iceland

    Wakati huo huo: Klabu ya Simba nayo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba wa mchezaji wake wa zamani mganda Abel Dhaira.
    "Kwetu sisi ni pigo kubwa sana, ni msiba mzito sana, umetufanya tupate fadhaa kubwa, lakini hatuna la kufanya zaidi ya kumtakia mapumziko mema ya milele,".
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara amesema watamkumbuka sana Dhaira kwa uwezo wake wa kudaka krosi na nidhamu yake iliyokuwa mfano kwa wachezaji wote waliokuwepo kipindi kile.

    "Tunawaomba familia ya marehemu iwe na subira kwenye kipindi hiki kigumu sana kwao,"amesema Manara. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DHAIRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top