Na Mwandishi Wetu, TANGA
KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwmaba hali ya hewa nzito ilichangia kufungwa mabao 2-0 na wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
“Hatukuwa na hali nzuri kimchezo, hali nzito ya hewa imetuathiri sana, tumecheza kukiwa na kiwango kikubwa cha joto, hata hivyo ndivyo matokeo ya soka yalivyo tulichokitarajia hakikuwa, tunakwenda Songea kwa mchezo mwingine, imani yangu tunaweza kupata ushindi huko” alisema.
Katika mchezo wa jana, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo zikiwa hazijafungana,licha ya kuwepo kwa mashambulizi kadhaa pande zote mbili ikiwemo lile la dakika ya 15 lililofanywa na Abdalah Juma wa City aliyefanikiwa kuwatoka mabeki wa Sports, lakini shuti lake likashindwa kulenga lango.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Sports kwani walipanga mashambulizi vizuri na kufanikiwa kulifikia lango la City mara kadhaa ikiwemo dakika 60 ambapo Omary Ibrahim alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kuongoza kwa mpira mzuri wa adhabu kufuati yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la City.
Mpira ukiwa unaelekea ukingoni Ibrahim tena alifanikiwa kufunga bao la pili kwa Sports baada ya kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Salum Isihaka na kufanikiwa kuwatoka walinzi wa City kisha kufunga akiwa pembeni kidogo mwa lango.

Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri kushoto amesema kwamba hali nzito ya hewa ilisababisha wafungwe jana Uwanja wa Mkwakwani |
Katika mchezo wa jana, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa timu hizo zikiwa hazijafungana,licha ya kuwepo kwa mashambulizi kadhaa pande zote mbili ikiwemo lile la dakika ya 15 lililofanywa na Abdalah Juma wa City aliyefanikiwa kuwatoka mabeki wa Sports, lakini shuti lake likashindwa kulenga lango.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Sports kwani walipanga mashambulizi vizuri na kufanikiwa kulifikia lango la City mara kadhaa ikiwemo dakika 60 ambapo Omary Ibrahim alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kuongoza kwa mpira mzuri wa adhabu kufuati yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la City.
Mpira ukiwa unaelekea ukingoni Ibrahim tena alifanikiwa kufunga bao la pili kwa Sports baada ya kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Salum Isihaka na kufanikiwa kuwatoka walinzi wa City kisha kufunga akiwa pembeni kidogo mwa lango.
0 comments:
Post a Comment