Dhaira siku za mwisho za uhai wake |
Kipa huyo wa kimataifa wa Uganda, amefariki akiwa nna umri wa miaka 28 nchini Iceland, ambako alikuwa anachezea klabu ya IBV Vestmannaeyjar.
Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Septemba 9, mwaka 1987, Dhaira amechezea klabu za AS Vita ya DRC, Express na URA za kwao, Uganda, Simba ya Tanzania na IBV ya Iceland.
Abbel Dhaira (kulia) akibadilishana mikataba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe wakati anasajiliwa Msimbazi mwaka 2013 |
Dhaira aliyechezea Simba kwa msimu mmoja wa 2013/2014 kabla ya kurejea Ulaya, alianza kupatiwa matibabu mapema mwaka huu baada ya klabu yake, IBV Vestmannaeyjar kuchangisha fedha kwa ajili hiyo, lakini wakati huo hali yake tayari ilikuwa mbaya sana.
Dhaira, alianza kuchezea timu ya taifa ya Uganda mwaka 2009 na akacheza Kombe la CECAFA Challenge mwaka 2012, ambako alikimbizwa hospitali na kulazwa baada ya kuzimia kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake. Pole kwa familia yake na Waganda wote. Mungu ampumzishe kwa amani Dhaira. Mbele yake, nyuma yetu. Amin.
0 comments:
Post a Comment