// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KILA LA HERI, AZAM, YANGA NA JKU MICHUANO YA AFRIKA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KILA LA HERI, AZAM, YANGA NA JKU MICHUANO YA AFRIKA LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 12, 2016

    KILA LA HERI, AZAM, YANGA NA JKU MICHUANO YA AFRIKA LEO

    WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Yanga, JKU na Azam wote wana mechi za ugenini leo.
    Yanga wanacheza na APR Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC wanacheza na Bidvest Wits, Uwanja wa Bidvest mjini Johannesburg, Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho.

    JKU ya Zanzibar itakuwa Uwanja wa Namboole mjini Kampala, Uganda kumenyana na wenyeji SC, Villa katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho.
    Tayari Mafunzo ya Zanzibar imekwishaipa mkono wa kwaheri michuano ya Ligi ya Mabingwa, baada ya kutolewa na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Raundi ya Awali.
    Azam FC walifika Johannesburg Jumatano, wakati Yanga waliingia Kigali Alhamisi na zote zimekuwa na muda mzuri wa maandalizi ya mwisho ugenini.
    Makocha wa timu zote, Stewart John Hall, Muingereza anayeinoa Azam FC na Hans van der Plijm, Mholanzi anayefundisha Yanga SC wamewaahidi Watanzania kufanya vizuri leo ugenini.
    Ikumbukwe timu zizo zitarudiana na wapinzani wao hao mwishoni mwa wiki ijayo Dar es Salaam kusaka tiketi ya kwenda hatua ya 16 Bora.
    BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE inazitakia kila la heri timu zote hizo ambazo leo zinapeperusha bendera ya nchi.   Mungu ibariki Tanzania. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA LA HERI, AZAM, YANGA NA JKU MICHUANO YA AFRIKA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top