SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeifungia Chad kushiriki mechi za kufuzu za fainali zijazo za Mataifa ya Afrika na kuitoza faini ya dola za Kimarekani 20,000.
Kwa mujibu wa kanuni ya 59 ya mashindano hayo; “Chama (Shirikisho la soka la nchi) chochote kinachojitoa baada ya kuanza kucheza mechi kitatozwa fainai ya dola 20,000. Pia hawataruhusiwa kucheza michuano inayofuata ya AFCON”.
CAF leo ilipokea barua ya Shirikisho la Soka Chad kujitoa katika Kundi G kwenye mbio za AFCON ya Gabon kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo kwa sasa na kwamba hawatakuwa na fedha za kusafiri kwenda kucheza mechi zao.
Na kwa mujibu wa kanuni za mashindano timu inapojitoa katika hatua ya kufuzu kwenye makundi matokeo yake yote yanafutwa. Sasa kila timu, Misri, Nigeria na Tanzania inapoteza pointi tatu ilizovuna kwa Chad na mabao yote.
Na Chad wamejitoa siku moja tu kabla ya mchezo wa marudiano na wenyeji Tanzania, uliopangwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Chad inajitoa baada ya kukamilisha mechi tatu za mzunguko wa kwanza, ikifungwa zote 2-0 na Nigeria ugenini, 5-1 na Misri nyumbani na 1-0 na Tanzania nyumbani Jumatano.
Sasa Kundi G linabaki na timu tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Misri.
MSIMAMO WA KUNDI G BAADA YA CHAD KUJITOA
Timu
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
Misri
|
2
|
1
|
1
|
0
|
4
|
1
|
+3
|
4
|
Nigeria
|
2
|
0
|
2
|
0
|
1
|
1
|
0
|
2
|
Tanzania
|
2
|
0
|
1
|
1
|
0
|
3
|
-3
|
1
|
Wenyeji Tanzania walikuwa kambini hoteli ya Urban Rose, katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa maandalizi tangu warejee kutoka D’jamena, Chad Alfajiri ya Ijumaa baada ya mchezo wa kwanza walioshinda 1-0 Jumatano iliyopita.
Na kwa mujibu wa uamuzi uliofikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF Januari 15 mwaka jana, kundi lolote ambalo litabaki na timu tatu litatoa timu moja tu ya kufuzu kwenye fainali za AFCON, maana yake sasa Kundi G halitatoa 'Best Loser'.
Misri inaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi mbili, wakati Tanzania inashika mkia kwa pointi yake moja.
Misri na Nigeria wanarudiana Jumanne Cairo baada ya kutoa sare ya 1-1 Jumapili Kaduna.
0 comments:
Post a Comment