Na Prince Akbar, D’JAMENA
KIPA Aishi Manula ataanza langoni leo katika mchezo wa Kundi G dhidi ya wenyeji Chad Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini hapa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
Kocha Charles Boniface Mkwasa amemuanzisha kipa huyo wa Azam FC badala ya Ally Mustafa ‘Barthez’ wa Yanga, zote za nyumbani Tanzania ambaye siku za karibuni amekuwa kipa wa kwanza.
Na Manula leo atalindwa na Shomary Kapombe kulia, Mwinyi Haji Mngwali kushoto, wakati mabeki wa kati watakuwa ni Erasto Nyoni na Kevin Yondan.
Viungo watakuwa ni Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Farid Mussa, wakati washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta na Thomas Uliwengu na Farid Mussa.
Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kufufua matumaini ya kwenda AFCON ya mwakani, baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za kwanza za kundi hilo, ikifungwa 3-0 na Misri mjini Cairo na kulazimishwa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam mwaka jana.
Misri ambayo itakuwa mwenyeji wa Nigeria leo, ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita baada ya kuzifunga Chad na Tanzania, wakati Super Eagles yenye pointi nne ni ya pili. Timu hizo zitarudiana siku nne baadaye, Chad inayoshika mkia Kundi G ikiwa haina pointi ikisafiri kwenda Dar es Salaam na Misri ikisafiri kwenda Nigeria.
Kikosi cha Stars leo; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali, Erasto Nyoni Kevin Yondani, Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Thomas Uliwengu na Farid Mussa.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mohamed Hussein, David Mwantika, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, John Bocco na Deus Kaseke.
Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Ibariki Taifa Stars. Amin.

Aishi Manula anaanza langoni leo Taifa Stars ikimenyana na Chad |
Mbwana Samatta (kulia) leo ataichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza kama Nahodha |
Viungo watakuwa ni Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Farid Mussa, wakati washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta na Thomas Uliwengu na Farid Mussa.
Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kufufua matumaini ya kwenda AFCON ya mwakani, baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za kwanza za kundi hilo, ikifungwa 3-0 na Misri mjini Cairo na kulazimishwa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam mwaka jana.
Misri ambayo itakuwa mwenyeji wa Nigeria leo, ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita baada ya kuzifunga Chad na Tanzania, wakati Super Eagles yenye pointi nne ni ya pili. Timu hizo zitarudiana siku nne baadaye, Chad inayoshika mkia Kundi G ikiwa haina pointi ikisafiri kwenda Dar es Salaam na Misri ikisafiri kwenda Nigeria.
Kikosi cha Stars leo; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali, Erasto Nyoni Kevin Yondani, Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Thomas Uliwengu na Farid Mussa.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mohamed Hussein, David Mwantika, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, John Bocco na Deus Kaseke.
Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Ibariki Taifa Stars. Amin.
0 comments:
Post a Comment