// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YASONGA MBELE KOMBE LA TFF BAADA YA KUIFUNGA 2-1 JKT MLALE TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YASONGA MBELE KOMBE LA TFF BAADA YA KUIFUNGA 2-1 JKT MLALE TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 24, 2016

    YANGA SC YASONGA MBELE KOMBE LA TFF BAADA YA KUIFUNGA 2-1 JKT MLALE TAIFA

    YANGA SC imetinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya kuifunga JKT Mlale mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mlale JKT ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao jioni ya leo kupitia kwa Shaaban Mgandila dakika ya 21 akimalizia krosi maridadi ya Edward Songo.
    Yanga SC ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake, Paul Nonga dakika ya 38 aliyemalizia pasi ya winga Godfrey Mwashiuya.
    Thabani Kamusoko (kushoto) ameifungia bao ushindi Yanga leo

    Yanga SC walipata bao la ushindi dakika ya 58 kupitia kwa kiungo wake Mzimbabwe, Thabani Kamusoko aliyemalizia tena krosi ya winga machachari, Mwashiuya.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’ Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Salum Telela/Thabani Kamusoko dk54, Matheo Anthony/Donald Ngoma dk46, Paul Nonga/Malimi Busungu dk59 na Godfrey Mwashiuya. 
    JKT Mlale; Noel Murish, Lucas Chapanga, Gerimanius Chindera, Said Ngapa, Frank Tesha, Othman Mhagama, Shaaban Mgandila, Omar Mnubi, Richard Mwadiga, Edward Songo na Alex Sethi/Raphael Siame dk50. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YASONGA MBELE KOMBE LA TFF BAADA YA KUIFUNGA 2-1 JKT MLALE TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top