MCHEZAJI aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Italia, Fabio Cannavaro amefukuzwa ukocha wa klabu ya Al Nasir ya Saudi Arabia baada ya miezi minne tu ya kuwa kazini.
Hiyo inafuatia kipigo cha mabao 4-3 kutoka Najran jana, ambacho kinawaangushia mabingwa hao watetezi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, zikiwa zimebaki mechi 10 kufikia tamati ya msimu.
Beki huyo wa zamani, ambaye aliiongoza nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 na pia alizichezea kwa mafanikio klabu za Juventus ya Italia na Real Madrid ya Hispania, ameiwezesha timu hiyo kushinda mechi sita tu kati ya 14 alizokuwa kazini.
Fabio Cannavaro amefukuzwa ukocha wa klabu ya Al Nasir ya Saudi Arabia baada ya miezi minne tu ya kuwa kazini
Hiyo inakuwa klabu ya pili Cannavaro kuondolewa tangu aanze ukocha, baada ya awali kufukuzwa pia na mabingwa wa China, Guangzhou Evergrande baada ya miezi michache tu ya kuwa kazini.
Baada ya kuajiriwa Oktoba mwaka jana, Cannavaro alipewa mechi 22 kuhakikisha anaisaidia Al Nassr kutetea ubingwa wa Saudi Pro League.
0 comments:
Post a Comment