// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TEGETE APIGA MBILI, MWADUI YAUA 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF, MBEYA CITY IMEBAKI JINA, YACHAPWA 2-1 NA PRISONS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TEGETE APIGA MBILI, MWADUI YAUA 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF, MBEYA CITY IMEBAKI JINA, YACHAPWA 2-1 NA PRISONS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 27, 2016

    TEGETE APIGA MBILI, MWADUI YAUA 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF, MBEYA CITY IMEBAKI JINA, YACHAPWA 2-1 NA PRISONS

    MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF
    Februari 24, 2016
    Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
    Februari 26, 2016
    Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
    Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
    Februari 27, 2016
    Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 
    Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
    Kesho; Februari 28, 2016
    Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 
    Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
    J’tatu Februari 29, 2016
    Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)
    Jerry Tegete amefunga mabao mawili leo Mwadui FC ikiilaza 3-1 Rhino Rangers 

    Na Waandishi Wetu
    TIMU za Mbeya City na Mwadui FC zimetinga Robo Fainali ya Kombe ka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya ushindi wa nyumbani leo.
    Prisons imewafunga ndugu zao, Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine, huo ukiwa mchezo wa pili mfululizo timu hiyo inapoteza chini ya kocha Mmalawi, Kinnah Phiri baada ya Jumatano kufungwa 3-0 na Azam katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Prisons walianza kupata bao dakika ya 39 kupitia kwa mshambuliaji wake, Mohammed Mkopi aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Sam Kimenya, kabla ya Mbeya City kusawazisha kupitia kwa Joseph Mahundi dakika ya
    Shujaa wa Priosns alikuwa ni Benjamin Asukile aliyefunga bao la ushindi dakika ya 82 baada ya kupiga mpira mrefu uliompita kipa Mganda wa Mbeya City, Hannington Kasyebula ambaye alikuwa amesogea mbele ya lango lake.
    Uwanja wa Mwadui Complex, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerson John Tegete amefunga mabao mawili, Mwadui FC ikiilaza 3-1 Rhino Rangers ya Tabora. Bao lingine la Mwadui limefungwa na Rashid Mandawa. 
    Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili ya hatua ya 16 Bora, Simba SC wakiikaribisha Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wenyeji Toto African wataikaribisha Geita Gold ya Geita.
    Mechi za 16 Bora ya michuano hiyo, zitahitimishwa keshokutwa kwa mchezo mmoja, kati ya wenyeji Panone FC dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
    Prisons na Mwadui zinafanya idadi ya timu zilizotinga Robo Fainali za michuano hiyo hadi sasa kufika nne, baada ya Yanga kuitoa JKT Mlale kwa kuifunga 2-1 Februari 24, Ndanda FC kuwatoa waliokuwa wanashikilia taji, JKT Ruvu kwa kuwafunga 3-0 na Coastal Union iliyoifunga 1-0 Mtibwa Sugar juzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TEGETE APIGA MBILI, MWADUI YAUA 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF, MBEYA CITY IMEBAKI JINA, YACHAPWA 2-1 NA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top