// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAWANIA TIKETI YA MICHUANO YA AFRIKA LEO, WANAMENYANA NA SINGIDA UNITED TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAWANIA TIKETI YA MICHUANO YA AFRIKA LEO, WANAMENYANA NA SINGIDA UNITED TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 28, 2016

    SIMBA WAWANIA TIKETI YA MICHUANO YA AFRIKA LEO, WANAMENYANA NA SINGIDA UNITED TAIFA

    MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF
    Februari 24, 2016
    Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
    Februari 26, 2016
    Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
    Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
    Februari 27, 2016
    Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) 
    Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
    Leo; Februari 28, 2016
    Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 
    Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
    Kesho; Februari 29, 2016
    Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)
    Wakongwe; Nyota watatu wazoefu wa Simba SC, kutoka kulia Justice Majabvi, Awadh Juma na Mussa Mgosi wanatarajiwa kuibeba timu yao leo mbele ya Singida United

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MICHUANO ya Kombe ka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili ya hatua ya 16 Bora.
    Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabingwa wa mwaka 2000 wa Kombe hilo, Simba SC watakuwa wenyeji wa Singida United ya Singida, wakati Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wenyeji Toto African wataikaribisha Geita Gold ya Geita.
    Singida inachagizwa na mafanikio ya kupandea Daraja la Kwanza kutoka la Pili wiki iliyopita, wakati Simba ina hasira ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa mahasimu, Yanga wiki iliyopita.
    Mechi za 16 Bora ya michuano hiyo, zitahitimishwa kesho kwa mchezo mmoja, kati ya wenyeji Panone FC dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
    Timu zilizotinga Robo Fainali za michuano hiyo hadi sasa ni nne, ambazo ni Yanga iliyoitoa JKT Mlale kwa kuifunga 2-1 Februari 24, Ndanda FC iliyowatoa waliokuwa wanashikilia taji, JKT Ruvu kwa kuwafunga 3-0, Coastal Union iliyoifunga 1-0 Mtibwa Sugar juzi, Prisons iliyowafunga 2-1 Mbeya City na Mwadui iliyowafunga 3-1 Rhino Rangers.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAWANIA TIKETI YA MICHUANO YA AFRIKA LEO, WANAMENYANA NA SINGIDA UNITED TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top